Marufuku kutumia ‘Drones’ bila kibali

Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imepiga marufuku urushwaji angani wa vifaa vya kieletroniki visivyo na rubani (drones) bila kupata kibali maalum. Taarifa ya TCAA iliyotolewa kwa vyombo vya habari, imesema kuwa, kwa taasisi au mtu binafsi kufanya majaribio au kurusha drones, ni lazima apate idhini ya Wizara ya Ulinzi na Usalama pamoja na…