Salah avunja rekodi ya dau la usajili Liverpool

Liverpool wamekamilisha dili la usajili winga Mohamed Salah, kutoka As Roma ya Italia, kwa dau la Pauni million 39. Usajili wa winga huyu umevunja rekodi ya usajili kwa wachezaji waliowahi sajiliwa na timu hiyo ambapo usajili wa gharama zaidi ulikuwa wa mshambuliaji Andy Carrol, aliposajiliwa kwa dau la pauni milioni 35 mwaka 2011. Salah raia…

Zaidi ya wafungwa 900 watoroka gerezani DRC

Gavana wa jimbo la Kivu ya Kaskazini Julien Paluku amesema zaidi ya wafungwa 900 wametoroka baada ya kutokea shambulizi na kuvunja gereza moja huko Congo DRC. Watu 11 wameuawa katika tukio hilo Kaskazini Mashariki mwa mji wa Beni. Haijajulikana ni nani haswa aliyefanya shambulizi hilo. Mwanaharakati mmoja anasema kwa makundi mengi yaliyojihami yanayojulikana kama Mai-Mai…

Kasisi aliyewalisha watu nyoka Afrika Kusini, afika Nigeria

Kasisi mmoja anayejiita nabii na ambaye alisababisha utata nchini Afrika Kusini, mwaka 2015, baada ya kutuhumiwa kuwafanya watu kula nyoka, panya na nywele ameonekana kwenye ibada nchini Nigeria Kasi huyo alioneaka katika ibada iliyoongozwa na mhubiri maarufu wa runinga nchini Nigeria TB Joshua mjini Lagos. Bw. Joshua ameandika katika mtandao wake wa kijamii kumhusu Mchungaji…

Mwanamke akamatwa China akiwa na mikoba iliyotengenezwa kwa cocaine

Maafisa wa forodha mjini Shanghai nchini China, wanasema kuwa wamemkamata mwanamke ambaye alijaribu kusafirisha mikoba miwili hadi nchini Uchina, ambayo ilikuwa imetengenezwa kwa kutumia dawa ya kulevya ya cocaine. Mwezi Februari mamlaka za viwanja vya ndege katika moja ya viwanja vya kimataifa mjini humo zilikagua kwa njia ya x-ray mkoba wa mwanamke ambaye alikuwa amesafiri…