Muigizaji azungumza kuhusu ”mauaji” ya Trump

Muigizaji wa filamu Johny Depp alitishia kumuua rais wa Marekani Donald Trump wakati wa hotuba katika sherehe za Glastonbury. Je unaweza kumleta Trump hapa? Aliwauliza mashabiki huku akizindua filamu yake ya The Libertine. Baada ya kuzomwa na mashabiki aliongezea: Hamukuelewa kabisa ni lini muigizaji alimuua rais? Nataka kuweka wazi ,aliongezea. ”Mimi ni muigizaji. Ninadanganya ili…

Zaidi ya wafungwa 900 watoroka gerezani DRC

Gavana wa jimbo la Kivu ya Kaskazini Julien Paluku amesema zaidi ya wafungwa 900 wametoroka baada ya kutokea shambulizi na kuvunja gereza moja huko Congo DRC. Watu 11 wameuawa katika tukio hilo Kaskazini Mashariki mwa mji wa Beni. Haijajulikana ni nani haswa aliyefanya shambulizi hilo. Mwanaharakati mmoja anasema kwa makundi mengi yaliyojihami yanayojulikana kama Mai-Mai…

Trump aisifu Saudi Arabia kwa kuitenga Qatar

Rais Trump ameungana na nchi ya Saudi Arabia katika mgogoro wa kidiplomasia unaoendelea na Qatar, huku akiusifu msimamo wa nchi hiyo ya tawala ya kifalme wa kuitenga nchi jirani baada ya Qatar kutuhumiwa kusaidia kifedha makundi yenye msimamo mkali. Trump ameandika katika ukurasa wake wa Twitter kwamba hatua hiyo inaweza kuwa ndio mwanzo wa kutokomeza…