Marufuku kutumia ‘Drones’ bila kibali

Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imepiga marufuku urushwaji angani wa vifaa vya kieletroniki visivyo na rubani (drones) bila kupata kibali maalum.


drone

Taarifa ya TCAA iliyotolewa kwa vyombo vya habari, imesema kuwa, kwa taasisi au mtu binafsi kufanya majaribio au kurusha drones, ni lazima apate idhini ya Wizara ya Ulinzi na Usalama pamoja na Mamlaka hiyo.

Taarifa hiyo iliyosainiwa na Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Hamza Johari imefafanua kuwa uendeshaji wa shughuli zote za anga nchini uko chini ya Mamlaka hiyo kwa mujibu wa sheria na kanuni zilizopo.

Tangazo hilo linakuja wakati ambapo kumekuwa na urushwaji wa drones unaofanywa na watayarishaji wa video za muziki kwa lengo la kuchukua picha za juu, pamoja na taasisi mbalimbali zinazochukua matukio husika hasa yanapofanyika katika maeneo ya wazi.

Drones zilitumika zaidi katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 ambapo mikutano ya kampeni za wanasiasa ilikuwa ikipigwa picha za juu kuonesha umati uliohudhuria.

Mjg4ODk4MA

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s