Salah avunja rekodi ya dau la usajili Liverpool

Liverpool wamekamilisha dili la usajili winga Mohamed Salah, kutoka As Roma ya Italia, kwa dau la Pauni million 39.

Mohamed Salah – akiwa Roma Itali

Usajili wa winga huyu umevunja rekodi ya usajili kwa wachezaji waliowahi sajiliwa na timu hiyo ambapo usajili wa gharama zaidi ulikuwa wa mshambuliaji Andy Carrol, aliposajiliwa kwa dau la pauni milioni 35 mwaka 2011.

Salah raia wa Misri mwenye umri wa miaka 25 amesaini mkataba wa miaka mitano kuweza kutumikia Liverpool.

”Ninafuraha sana kuwepo hapa nitajitoa kwa asilimia mia moja na nitatoa kila kitu kwa ajili ya klabu hii, kiukweli nataka kushinda kitu nikiwa na timu hii”, alisema Salah baada ya kukamilisha usajili huo.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s