PICHA KUTOKA AFRIKA ZILIZOVUTIA WIKI HII

Baadhi ya picha zilizovutia kutoka Afrika na Waafrika wengineo mahala tofauti ulimwenguni wiki hii.

_96412400_model

Wanamitindo wajiandaa kufanya maonyesho kwenye wiki ya mitindo ya Afrika katika mji mkuu wa Nigeria, Lagos, siku ya Jumamosi.

_96412401_models2

Hafla hilo huonyesha mitindo bora zaidi ya Kiafrika, kutoka Nigeria, Senegal, Cameroon, Ghana na Zambia.

_96412402_models3

Siku ya Alhamisi nchini Misri, kasuku kutoka familia ya macaw aonekana katika hifadhi ya wanyama ya Africano, katika barabara ya jangwani kati ya Cairo na Alexandria.

_96412403_floodsdarfur

Huku punda akivuta mizigo ya watu walioathiriwa na mafuriko katika eneo la Darfur nchini Sudan siku ya Jumamosi.

_96412404_beachphotoman

Katika eneo la Cape Town Afrika Kusini siku ya Jumatano, mpiga picha avumilia dhoruba ili kupata picha ya mawimbi.

_96412405_sa2

Ilikuwa ni dhoruba kali zaidi kuwahi kuonekana Cape Town kwa miongo mitatu.

_96412406_ochestra

Siku ya Jumanne, wanabendi kutoka Tunisia wanawatumbuiza watu kwenye tamasha katika mji mkuu wa Tunis.

_96412407_drumbeaters

Tamasha hiyo ya kila mwaka hufanyika wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadan na ni sherehe ya dhehebu la Sufi

_96412408_albino

Kaskazini mashariki mwa Nigeria, Mwanamke anangojea mgao wa chakula katika kambi iliyo katika pambizo la mji wa Maiduguri.

_96412409_settlement

Yeye ni miongoni mwa maelfu ya watu wanaoishi katika kambi hiyo ili kutoroka mashambulizi yanayotekelezwa na wapiganaji wa kundi la Boko Haram.

_96412460_themugabes

Siku ya Ijumaa, Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe na mkewe Grace wanatabasamu baada ya kuwasili mashariki mwa mji wa Marondera kuhudhuria mkutano wa kisiasa.

_96412461_mugaberally

Uliikuwa ni mkutano wa kwanza kati ya mikutano ya kisiasa aliyoandaa Mugabe, mwenye umri wa miaka 93 ya kuwashawishi wananchi wamuunge mkono katika uchaguzi mkuu utaofanyika mwaka ujao.

_96412462_rallypics

Ni mikutano inayowalenga vijana lakini hilo halikuwazuia walio wachanga moyoni kuhudhuria.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s