JE WAJU!?: Yai kwa siku inaonekana kusaidia watoto wadogo kuongeza kimo

Kula yai kwa siku kunaweza kuwasaidia watoto wadogo wenye utapiamlo kuongeza urefu kulingana na utafiti wa miezi sita huko Ecuador.

Haijalishi ikiwa ni yale yaliyo chemshwa, au ya kukaanga, na watafiti wanasema ni njia isiyo ghali ya kuzuia kudumaa.

Miaka miwili ya kwanza maishani ni ya muhimu sana kwa ukuaji na maendeleo na kudumaa kunaweza kuleta madhara makubwa.

Lishe duni ni sababu kubwa ya kudumaa, pamoja na maambukizi ya utotoni na magonjwa.

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani, WHO, watoto milioni 155 chini ya umri wa miaka mitano wamedumaa (wafupi kwa umri wao).

Wengi wao wanaishi katika nchi zilizo na mapato ya chini na ya kati na wataalamu wa afya wamekuwa wakitafuta njia za kukabiliana na suala hilo.

Lora Iannotti na wenzake walifanya majaribio katika nyanda za vijijini ya Ecuador na kuwapa watoto wadogo sana (wenye umri wa miezi sita hadi tisa) mayai, ili kuona kama yataweza kuwasaidia.

fehi218.gif

Nusu tu kati ya watoto 160 ambao walishiriki katika majaribio walilishwa yai kila siku kwa muda wa miezi sita – wengine walifuatiliwa tu kwa sababu za ulinganifu.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s