Kasisi aliyewalisha watu nyoka Afrika Kusini, afika Nigeria

Kasisi mmoja anayejiita nabii na ambaye alisababisha utata nchini Afrika Kusini, mwaka 2015, baada ya kutuhumiwa kuwafanya watu kula nyoka, panya na nywele ameonekana kwenye ibada nchini Nigeria

Kasi huyo alioneaka katika ibada iliyoongozwa na mhubiri maarufu wa runinga nchini Nigeria TB Joshua mjini Lagos.

Bw. Joshua ameandika katika mtandao wake wa kijamii kumhusu Mchungaji Penuel Mnguni, kuhudhuria ibada yake.

Gazeti la Afrika Kusini, Citizen, limemnukuu Bw. Mnguni akisema kuwa amebadilisha moyo wake, baada ya kujikuta ndani ya utata na habari zake kugonga vichwa vya habari duniani- huku akikamatwa na kuachiwa mara kwa mara

‘Nilianza kutizama runinga ya Emmanuel TV, kumsikiliza nabii TB Joshua, na nikafahamu kuwa, nilichokuwa nikifanya haikuambatana na maandiko. Nilifahamu kuwa lilikuwa shambulio. Nikaja hadi kwa TB Joshua ili anikomboe.” Amesema Bw. Mnguni.

Mashtaka dhidi ya Bw. Mnguni, yaliyowasilishwa na chama cha kupambana na dhuluma dhidi ya wanyama (Society for the Prevention of Cruelty to Animals), Afrika Kusini, yaliondolewa mnamo Julai mwaka 2015, kwa kukosa ushahidi.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s