Sera ya WCB: Marufuku msanii wa WCB kwenda club za usiku kula bata

Mtayarishaji wa muziki kutoka label ya WCB ya Diamond Platnumz, Laizer amesema kuwa moja kati ya sera za lebo hiyo, zinakataza wasanii pamoja na mtayarishaji huyo kwenda kwenye klabu za usiku kula bata.

Diamond akiwa na wasanii wake wa WCB.

Akiongea katika kipindi cha Twenzetu ya Times Fm wiki hii, Laizer amedai wasanii hao hawaruhusiwi kuingia club bila ruhusa maalum.

“Moja kati ya vitu ambavyo tunakatazwa ni kwenda klabu za usiku, hii hairuhusiwi kabisa,” alisema Laizer “Nadhani ni kwa sababu ya brand, haitakuwa kitu kizuri kuona brand inazurula tu usiku kwenye klabu na kama unavyojua klabu za usiku zina mambo mengi,” aliongeza.

Hata hivyo alisema kuwa wasanii hao wanaruhusiwa kuingia klabu kama kuna kazi au kuna mwaliko maalum utakaowasilishwa kwenye menejimenti kama mwaliko rasmi.

Endelea kubang tu na ngoma za WCB kwenye klabu ya usiku unayoikubali zaidi, lakini usitegemee kumuona Harmonize, Rich Mavoko, Raymond, Lava Lava hata bosi mwenyewe Chibu Dangote wakila bata karibu na wewe ndani ya klabu hizo bila mualiko maalum.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s