Serikali imegharamia Sanda pamoja na majeneza kwa ajili ya Wanafunzi wa Shule ya Lucky Vicent waliopoteza maisha kwenye ajali ya Bus….

Serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania imegharamia Sanda pamoja na majeneza kwa ajili ya Wanafunzi wa Shule ya Lucky Vicent waliopoteza maisha mapema jana kwenye ajali iliyokuwa ikihusisha safari ya kimasomo.

Akitoa taarifa hiyo leo Meya wa Jiji la Arusha , Mh. Calist Lazaro amesema kuwa taarifa za awali zinaonyesha kuwa tayari Serikali imekwishalipia gharama za majeneza na sanda ya kuhifadhia miili ya marehemu ambao kesho wanatarajiwa kufanyiwa ibada katika Uwanja wa mpira wa Sheikh Amri Abeid.

Aidha, Mh. Lazaro amesema kuwa viongozi mbali mbali wakiwemo mawaziri pamoja na wabunge bado wanaendelea kukusanyika katika eneo la shule ya Lucky Vicent  kwa ajili ya kikao na baadae majira ya saa tisa au kumi taarifa rasmi ya serikali itatolewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s