VIDEO: Afande Sele ameeleza alivyoishi na baba mzazi wa Belle 9

April 18, 2017 zilitangazwa taarifa za kifo cha mzee Damian Nyamoga ambaye ni baba mzazi wa Belle 9 aliyefariki usiku wa kuamkia April 18, 2017 akiwa hospitali akipatiwa matibabu baada ya kugongwa na pikipiki mjini Morogoro.

Mzee Nyamoga amezikwa April 19, 2017 mjini Morogoro ambapo moja kati ya mastaa walioguswa na msiba huo ni Mfalme wa Hip Hop Tanzania Afande Sele ambaye licha ya kuwa mtu wa karibu wa familia ya marehemu, ameiambia Ayo TV na millardayo.com namna walivyoishi na mzee Nyamugo.

“Nilichojifunza ni kitu kimoja, ambacho kwangu mimi ndiyo kina thamani zaidi kuliko vitu vyote, utu wema. Unaweza kuwa na majumba na mali za kila aina, lakini kama unakosa utu wema, basi we thamani yako inakuwa haipo katika maisha.

“Unaweza kuona katika mazishi yake yalivyo, watu walivyohudhuria, walivyojaa hapa; akina mama, watoto, kila mtu yuko hapa, kwa sababu ya kitu kinaitwa utu wema siyo kwa ajili ya mali za huyu mzee.” – Afande Sele.

Bonyeza play kwenye video hapa chini kutazama…

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s