Moja kati ya stori kubwa mitandaoni ni kuhusu staa wa Bongofleva Shilole kugeukia katika ujasiliamali mbali na muziki ambapo amefungua mgahawa unaoitwa Shishi Trump kwa lengo la kujiongezea kipato.

Usiku wa April 14 2017 kupitia The Weekend Chart Show ya Clouds TV, Shilole alizungumzia maendeleo ya biashara yake hiyo akiweka wazi kiwango cha mshahara anachowalipa wafanyakazi wake 10 waliopo mgahawani kuwa ni Shilingi 200,000 kila mmoja lakini mtu wa jikoni analipwa zaidi.

>>>”Nimeajiri watu kumi na kila mfanyakazi wangu hapa analipwa Laki Mbili japo inategemea. Mfanyakazi wa jikoni ndio analipwa hela nyingi, ila mimi sijilipi. Nawa-manage vizuri maana tunapata wateja wengi na wafanyakazi wanajituma. Kuna mtu kama Pendo ambaye nimetoka naye mbali, so, anafanya kazi vizuri. Ananifurahisha.” – Shilole

Katika hatua nyingine Shilole alielezea tukio la kuvunjwa kwenye eneo la biashara yake na watu wasiofahamika kisha kuiba TV, Radio, vinywaji na baadhi ya vitu:>>>

”Alikuja meneja wangu kashika mikono kichwani, akanieleza kuwa tumeibiwa, vinywaji vimechukuliwa vyote. Ikabidi nije naye ofisini na kukuta watu wameiba TY, Radio na vinywaji. Nilipata hasara ila sikufunga biashara. Jioni nilienda kununua vinywaji na biashara ikaendelea.” – Shilole.

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s