VIDEO: Mbunge wa zamani aliyezushiwa kifo mapema leo amezungumza

Asubuhi mapema April 13, 2017 kulizuka taarifa ambazo zilisambaa kwenye mitandao ya kijamii zikieleza kifo cha Mwanasiasa mkongwe na Mbunge wa zamani wa Kwela ‘CCM’, Dkt. Crisant Mzindakaya.

Taarifa hizo zilieleza kuwa Dkt. Mzindakaya alifariki akiwa kwenye matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Dkt. Crisant Majiyatanga Mzindakaya, aliingia Bungeni kwa mara ya kwanza mwaka 1965 kama Mbunge wa Jimbo la Ufipa Kusini, lakini mbio zake ziliingia doa mwaka 1981 baada ya Mahakama kumvua Ubunge kutokana na ushindi wake wa mwaka 1980 kudaiwa kutumia faulu. Mwaka 1982 alirejea tena Bungeni baada ya kuteuliwa na Rais kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya ambapo wakati huo wakuu wa mikoa walikuwa wanaingia Bungeni moja kwa moja.

Ayo TV na millardayo.com ilifika katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete na kumkuta mzee Mzindakaya akiwa mzima huku akiendelea vizuri ambapo kulikuwa na uwezokano wa kumruhusu.

Bonyeza play kutazama…

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s