VIDEO: KRC Genk yakina Samatta imekubali kipigo vs Celta Vigo ugenini

Mtanzania Mbwana Samatta usiku wa April 13 2017 akiwa na timu yake ya KRC Genk aliingia uwanjani kucheza game yake ya 11 ya Europa League toka waanze hatua ya makundi dhidi ya Celta Vigo katika uwanja wa Balaidos Hispania.

Mchezo huo ulikuwa ni robo fainali ya kwanza na KRC Genk waliyokuwa ugenini wamejikuta wakipoteza mchezo wao wa kwanza baada ya kucheza game sita mfululizo bila kupoteza katika mashindano yote, Genk wamefungwa magoli 3-2, katika historia Genk na Celta Vigo ndio wamekutana kwa mara ya kwanza.

Magoli ya KRC Genk yalifungwa na Jean Boetius dakika ya 10 na Thomas Buffelaliyeingia akitokea benchi dakika ya 68, kwa upande wa wenyeji magoli yao yalifungwa na Pione Sisto dakika ya 15, Iago Aspas dakika ya 17 na John Guidetti dakika ya 38, kipigo hicho kinailazimu Genk katika mchezo wa marudiano Luminus Arena April 20 itabidi wapate ushindi wa kuanzia goli 1-0 ili wafuzu nusu fainali.

Kwa upande wa Mbwana Samatta amecheza game hiyo kwa dakika zote 90 na kutimiza jumla ya dakika 756 alizocheza katika mechi zote 11, akifunga magoli mawili, assist moja na akipiga jumla ya mashuti 7 yaliyolenga goli, Samatta baada ya kufunga katika mechi 5 mfululizo za Genk leo amecheza game yake ya pili bila kufunga.

View image on Twitter

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s