Serikali yapigilia msumari wa moto biashara ya mayai

Serikali imesema kuanzia mwaka 2013 hadi 2017 imeteketeza vifaranga 67,500 vilivyoingizwa nchini kinyume na sheria kuepuka ugonjwa hatari wa mafua ya ndege.

baby-chick-and-an-egg.jpg

Kauli hiyo imetolewa Jumatatu hii mapema bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, William Tate Ole Nasha wakati akijibu swali la mbunge wa Ukonga Mwita Waitara lililohoji,

“Baadhi ya wakazi wa Ukonga wanafuga mayai na wengine wanatengeneza chakula cha mifugo na shughuli zingine zinazowainulia kipato. Je, serikali ina mpango gani wa kuzuia uingizaji wa mayai ya kuku kutoka nje.? – Mwita Waitara

Majibu yake yalikuwa, “Kuanzia mwaka 2006 serikali iliweka katazo kuingiza kuku ili kudhibiti ugonjwa hatari wa mafua ya ndege. Sheria ya magonjwa wanyama namba 17 2013 na kanuni zake na 2007 na 2010 zinatumika kudhibiti na kukagua uingizwaji wa mpakani, bandari na viwanja vya ndege hakuna mwekezezaji yeyote anayeruhusiwa kupewa kibali cha kuingiza vifaranga au mayai nchini kwaajili ya biashara na katika kusimamia hili kuanzia mwaka 2013 mpaka 2017 vifaranga 67,500 vilivyoingizwa nchini kinyume na sheria viliteketezwa,” amesema Nasha.

“Serikali inasimamia ubora wa malighafi za kusindika vyakula vya mifugo kupitia sheria za maeneo ya nyanda za malisho na rasilimali za vyakula vya wanyama namba 13 ya mwaka 2010.”

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s