VIDEO: Kipigo cha Arsenal kilichovunja rekodi ya Arsene Wenger April 10

Usiku wa April 10 2017 timu ya Arsenal ya England inayofundishwa na kocha Arsene Wenger ambaye kwa sasa mashabiki wengi wa Arsenal wanalalamikia aondoke katika timu hiyo kutokana na kutopatia mataji kwa zaidi ya miaka kumi sasa, usiku huo ilicheza dhidi ya Crystal Palace wakiwa ugenini.

Arsenal ambayo imezoeleka kutofanya vizuri katika Ligi Kuu England lakini haikosekani katika nafasi nne  za juu ambazo inawanapata nafasi ya kucheza Champions League, usiku wa April 10 2017 wamechezea kichapo cha magoli 3-0 kutoka kwa Crystal Palace game iliyochezwa katika uwanja wa Selhurst Park.

Magoli yakitiwa wavuni na Andros Townsend dakika ya 17, Yohan Cabaye dakika ya 63 na Luka Milivojevic kwa mkwaju wa penati dakika ya 68 na kuiacha Arsenal ikimaliza mchezo huo ikiambulia kumiliki mpira kwa asilimia 73 na Crystal Palace 27, kipigo hicho kinaifanya Arsenal kufungwa kwa mara ya kwanza mechi nne mfululizo za Ligi kwa mara ya kwanza chini ya Arsene Wenger.

Mechi nne ilizofungwa mfululizo za ugenini Arsenal na Chelsea 3-1, Liverpool 3-1, West Bromwich na leo imepoteza 3-0 dhidi ya Crystal Palace lakini hicho kinakuwa ni kipigo cha kwanza toka Arsenal ipate ushindi wa kwanza wa EPL April 6 2017 dhidi ya West Ham United baada ya siku 53 bila kupata ushindi, mfululizo wa matokeo hayo kuna hatarisha nafasi ya Arsenal kucheza Champions League msimu ujao.

Msimamo wa EPL ulivyo kwa sasa baada ya matokeo ya game ya Crystal Palace vs Arsenal usiku wa April 10 2017

C9FRluSXoAEaFea

Bofya hapa kuangalia magoli yote ya mechi hiyo Ayo Tv

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s