Nikki wa Pili ameingiwa na hofu baada ya Roma kutekwa

Ni April 8 2017 ambapo stori kubwa inayotrend ni kupotea kwa Roma Mkatoliki na wenzie watatu waliochukuliwa Tongwe Records na watu wasiojulikana na kupelekwa kusikojulikana huku hofu ikitawala miongoni mwa watanzania.

Kupitia Clouds 360 on Saturday ya Clouds TV Rapa staa kutoka ‘WEUSI’ Nikki wa Pili ameelezea juu ya habari za kutoweka kwa Roma Mkatoliki akisema ni jambo baya ambalo linaogopesha na kutia hofu.

>>>“Kwanza ni jambo la kuogopesha na kutia hofu. Roma amepotea, tumejua kwa sababu ni mtu maarufu hata mtu mwingine wa kawaida anaweza kupotea. Kwa hiyo, hili ni jambo ambalo halitakiwi katika nchi yetu. Kama wananchi na serikali tushirikiane kumpata jamaa na tukemee kabisa maana haki ya kwanza ya binadamu ni kuishi, na kuishi ni usalama.

“Kwa hiyo, mimi naamini hili ni jambo baya. Kwanza tuwatafute hawa watu, halafu tulindane maana sisi hatuna CCTV camera. So, tulindane maana ulinzi wetu sisi ni sisi wenyewe.

“Inanitia hofu katika maeneo mawili; kwanza, inanipa hofu kama msanii kwa sababu ni tasnia yetu, lakini pili, inanipa hofu kama binadamu maana binadamu yeyote anaweza kutekwa. So, inanipa hofu maeneo yote mawili.” – Nikki wa Pili.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s