Ombi la Idriss Sultan kwa Rais Magufuli kuhusu Roma

Baada ya msanii wa muziki Roma Mkatoliki kupotea katika mazingira ya kutatanisha akiwa katika studio ya Tongwe Records wasanii mbalimbali wameonesha kuguswa na kuamua kutumia mitandao yao ya kijamii kuonesha masikitiko yao, Leo April 7 kupitia mtandao wa Instagram Idriss Sultan alikua na haya ya kusema,

Hawa ni wasanii na ni maarufu, sitamani kujua ni wangapi tusiowajua waliopotea katika mfumo kama huu. Nina hofu sio kwa maisha yangu na uhuru wangu ila kwa kaka, dada, watoto, baba, mama na ndugu , wake, waume, na wapenzi wa watanzania wenzangu wasio na sauti niliyo nayo mimi –Idris Sultan

Mwenyezi Mungu hakunipa nilichonacho ili niishie kupimisha misuli na wenzangu nani zaidi, watu kama mimi ndio wa kwenda motoni haraka zaidi tukishaulizwa ulifanyia nini ulichopewa. Raisi Magufuli, waziri Mwakyembe na Mkuu wa mkoa Makonda nina imani hili lipo mezani kwenu naombeni mlitolee tamko zaidi ya “Uchunguzi unafanyika” –Idris Sultan

pia mlivalie njuga kuwapata ndugu zetu ili kutuliza amani ya hii nchi iliyopiganiwa iliyokuzwa kwa upendo na amani ya juu kabisa. We can’t call it the land of peace wakati ukilala hujui kama utaaamka sehemu unayoijua na ukiwa hata na hali yako ya kiafya ile ile.Idris Sultan

Leo ni Roma na Moni, kesho ni nani ? Kamanda Sirro sijasahau kabisa usalama wa huu mji upo mikononi mwako. Wake za hawa wawili wanaongea na watoto wao wanawaambia baba yupo ila amesafiri anarudi kesho. Kesho isipofika basi inshaallah tutajua Tanzania yetu ni nchi ya aina gani. Hata Mungu simuachii hili hatujalishindwa bado Idris Sultan

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s