Swali walilouliza Europa League kuhusu Mbwana Samatta leo

Tukiwa tunaelekea kutazama michezo ya kwanza ya robo fainali ya UEFA Europa League alhamisi ya April 13 2017, jina la mtanzania Mbwana Samatta limezidi kuchukua headlines katika michuano hiyo, Samatta na timu yake ya KRC Genk watacheza mchezo wao wa kwanza wa robo fainali dhidi ya Celta Vigo ya Hispania.

Leo kupitia ukurasa rasmi wa twitter account ya UEFA Europa League wamelitaja jina la mtanzania Mbwana Samatta kwa kumpost katika twitter account yao na kuuliza swali je huyu ni wa kumuangalia?hiyo ni baada ya Samatta kuonesha uwezo mkubwa akiwa na Genk katika mechi 5 zilizopita.

Samatta katika mechi tano zilizopita za KRC Genk za mashindano tofauti amefanikiwa kufunga jumla ya goli 6 hivyo Samatta kwa takwimu hizo anatajwa kama mchezaji wa kuangaliwa, Genk watacheza mchezo wao wa kwanza wa Europa League ugenini dhidi ya Celta Vigo nchini Hispania katika uwanja wa Balaidos saa 22:05 kwa saa za Afrika Mashariki.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s