Sehemu nane za utalii zinazostaajabisha na kuvunja rekodi duniani

Kila siku duniani kunaibuka vitu vya kushangaza na sehemu za kustaajabisha ambazo huongezeka na kuvutia umakini wa watu hasa watalii. Ikiwa ni kazi yangu kukuletea stori mbalimbali zinazotrend, leo April 6, 2017 nakusogezea stori ya maeneo 8 ambayo yanastaajabisha.

1: Kisiwa cha wanasesere Mexico

Ni kisiwa kinachopatikana Kusini mwa Mexico ambacho kwa mwaka hupata watalii zaidi ya Laki Nane. Kisiwa hiki kimepambwa kwa wanasesere wanaokadiriwa kufikia million 1 ambapo kwenye kila mti kumening’inizwa wanasesere ambao hupelekwa na watalii kila wanapotembelea na kufanya kisiwa kizima kijae wanasesere.

2: Hekalu la panya India

Hekalu hili limekua moja ya sehemu za kitalii zinayoingizia serikali ya India kiasi kikubwa cha pesa kwa mwaka. Linaaminika kuwa ni sehemu takatifu ambayo ina zaidi ya panya 20,000 ambao hupewa chakula na kuhudumiwa kwa heshima kubwa. Watalii hutembelea hekalu hili na kufanya ibada.

3: Duka la Prada

Duka hili la kifahari limejengwa katikati ya Jangwa mjini Texas, Marekani ambapo hakuna kiumbe yeyote anayeishi maeneo hayo na hakuna mteja atakayeweza kununua chochote katika duka hilo licha ya kuwa na bidhaa. Jambo la kushangaza zaidi ni kuwa halina milango wala madirisha. Mji wa Texas umelifanya duka hili kama sehemu ya watalii kutembea.

4: Makumbusho yaliyojengwa chini ya bahari

Ni makumbusho yaliyojengwa chini ya bahari mwaka 2009 na Mkurugenzi wa National Marine Park Jaime González kwa lengo la kuzuia kupotea kwa viumbe wa baharini waliokuwa wanapotea kwa kukosa makazi. Watalii wengi walivutiwa na masanamu hayo na mwaka 2015 makumbusho hayo yalifanywa sehemu ya utalii.

5: Handaki la mateso Urusi

Handaki hili ni sehemu ya mabaki yaliyohifadhiwa kama kumbukumbu na Wizara ya Utalii ya Urusi ambapo watalii kutoka sehemu mbalimbali duniani hutembelea na kuteswa kwa siku moja ili kujua mateso waliyopitia watu wakati wa Vita Baridi ‘Cold war.’

6: Ukuta wa Big G CarlifoRnia

Ukuta huu upo Carlifonia, Marekani ambapo inakadiriwa zaidi ya Big G zilizotafunwa zimebandikwa kwenye ukuta huu. Mwaka 1993 kabla ya kuwa sehemu ya utalii eneo hili lilikua ni theater, lakini watu mbalimbali walikuwa wakitafuna big g na kubandika ukutani kwa makusudi. Kadiri uongozi ulipokemea ndivyo watu walivyozidi kubandika ndipo mwaka 1999 ikabadilishwa matumizi na kuwa sehemu ya utalii.

7: Gereza Inveraray Scotland

Gereza Inveraray ambalo limejengwa mwaka 1820, ni sehemu inayopendwa kutembelewa na watalii duniani ambao hupata nafasi ya kufungwa jela kwa saa 24 wakipitia mateso kama mfungwa halisi aliyewahi kufungwa miaka ambapo ili kutoka ni lazima mtu atafute njia ya siri.

8Makumbusho ya nywele Uturuki

Makumbusho ya Avanos Turkey ni sehemu inayotembelewa na zaidi ya watalii million 1 kwa mwezi hivyo kujizolewa umaarufu mkubwa duniani. Watalii wanapotembelea makumbusho haya hukata nywele zao na kuzihifadhi ambapo inadiwa kuwa kwenye makumbusho hayo kuna zaidi ya nywele 16,000 tangu mwaka 1979.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s