Polisi DSM waeleza sababu za kufananishwa na TRA katika utendaji

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro leo April 5, 2017 ameeleza sababu za Jeshi hilo kufananishwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania ‘TRA’ katika utendaji wao wa kazi hasa katika ukusanyaji wa mapato.

Kamanda Sirro ametoa ufafanuzi huo mbele ya Waandishi wa Habari akisema kumeibuka maneno sehemu mbalimbali hasa mitandaoni wananchi wakidai kuwa Jeshi hilo limeacha kazi yake ya kulinda raia na mali zao na kufanya kazi ya kukusanya mapato ambayo hufanywa na TRA.

“Nimeona watu wengine wanazungumza kwenye mitandao kwamba Polisi wamekuwa kama TRA. Mimi niliweke vizuri, sheria zipo. ukiangalia katika sheria ya Usalama barabarani iko vizuri. Na kama umekamatwa na kosa ambalo tunaamini umekiuka makosa ya Usalama barabarani hatukulazimishi wewe kulipa ile faini. Kuna mawili; kama hauko tayari kulipa ile faini, utaratibu upo tunakupeleka Mahakamani.” – Kamanda Sirro.

Nimekushushia na link ya video hapa chini, kupitia Millardayo.com na Ayo Tv

Millardayo.com

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s