Viumbe watano wanaopewa heshima kubwa jeshini mbali na binadamu

Kwa kawaida wanyama hurahisisha maisha ya wanadamu kwakuwa walinzi wetu, chakula chetu na usafiri wetu lakini kuna baadhi ya wanyama na ndege walioweza kujiwekea heshima duniani hasa  kwenye sekta maalum za kijeshi na wameweza kupata nafasi za juu jeshini.

 1: Sir Nils Olav

Nils Olav ni ndege aina ya Penguin alipewa cheo mara ya kwanza mwaka 1972 na kuwekwa  kwenye timu ya walinzi wa mfalme Harald V Loudon wa Norway kwa sasa Sir Nils Olav ni Brigedia anapewa heshima zote za kijeshi ikiwemo kupigiwa saluti na kukagua jeshi.

pjimage-39

2: Treo

Ni mbwa aliyetumikia jeshi la Uingereza kuanzia mwaka 2001 mpaka 2015 , Trio ana medali zisizopungua 63, alipewa medali hizo baada ya kufaya kazi kubwa ya kutegua mabomu na kutambua mahali mabomu yalipo fichwa.

Dog-handler-431049

3: William of Orange.

William ni njiwa aliyekuwa mwanajeshi wa jeshi la Uingereza mwenye namba  MI14, mwaka 1944 William alipewa medali ya 21 baada ya kupeleka ujumbe uliyookoa vifo vya wanajeshi zaidi ya 2000 kwenye vita ya Arnhem wakati wa vita ya pili ya dunia.

a03c313793ffca258f5f34849aa07704

4: Taffy IV.

Huyu ni mbuzi aliyetumikia jeshi la Uingereza tangu mwaka 1775 Taffy IV alichukuliwa kwa mara ya kwanza mwaka 1774 na kuingizwa kwenye jeshi maalum la Uingereza alipokutwa anarandaranda porini, alipewa medali ya 14 ambayo ni medali maalum waliyopewa wanajeshi wa Uingereza wakati wa vita ya kwanza ya dunia (ww1).

0777960bba60d1af88bf9d2da68fba3b

5: LIN WANG

Ni tembo aliyekuwa mwanajeshi wa jeshi la China kuanzia mwaka 1942 Lin Wang alitumika kujenga majengo marefu ya jeshini, kusafirisha chakula wakati wa vita na alitumika kama kivutio kwa ajili ya kukusanya fedha wakati wa njaa kipindi cha vita alipewa medali 12 za kijeshi.

pjimage-1-8

 

source:
millardayo.com

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s